Taarifa zilizotufikia ambazo bado zipo chini ya kapeti ni kwamba Kampuni ya Clouds Media Group, imeamua kumfungilia mashitaka msanii nguli wa Bongo Fleva na kiongozi wa bendi ya Machozi, Judith Wambura Mbibo ‘Lady Jaydee’. Clouds imeamua kufungua mashitaka hayo baada ya Lady Jaydee kuchafua jina la kampuni hiyo na viongozi wake wawili wa juu ambao ni Mkurugenzi Mtendaji, Joseph Kusaga na Mkurugenzi wa Utafiti na Maendeleo, Ruge Mutahaba katika mitandao ya kijamii hivi karibuni. Lady Jaydee anatakiwa kuripoti katika Mahakama ya Kinondoni kukabiliana na tuhuma hizo hapo kesho.
Home »
» TANZANIA:CLOUDS FM MEDIA GROUP IMEAMUA KUMSWAGA MAHAKAMANI MSANII MAARUFU LADY JAYDEE:
No comments:
Post a Comment