Habari Mpya :
Home » , » MKE WA MTU ABAKWA NA KUNYONGWA CHARINZE KWA MWARABU

MKE WA MTU ABAKWA NA KUNYONGWA CHARINZE KWA MWARABU

Imeandikwa na Shamsi Mohamed on Saturday, December 14, 2013 | 3:32 AM

Mwanamke mkazi wa Chalinze, Mkoa wa Pwani, Moshi Rashid (43)
amefanyiwa unyama uliopitiliza na watu wasiojulikana baada ya
kumbaka na kumnyonga, inauma sana kwa kweli!
Mwanamke
mkazi wa Chalinze, Mkoa wa Pwani, Moshi Rashid (43) amefanyiwa
unyama uliopitiliza na watu wasiojulikana baada ya kumbaka na
kumnyonga.
Tukio hilo la kutisha lilijiri usiku wa Desemba 7, mwaka huu
Chalinze Kwamwarabu ambapo mwanamke huyo alikwenda
kujumuika na ndugu na majirani katika mkesha wa ngoma ya
kuwatoa wari siku ya Jumapili.
Eneo la tukio Chalinze
Kwamwarabu.
Mkasa huu unasimuliwa kwa majonzi mazito na mdogo wa
marehemu ambaye alikuwa mshehereshaji wa shughuli hiyo ‘MC’,
Siwema Rashid.
Alisema: “Mpaka sasa tunashindwa kuelewa kilichotokea maana
siku ya tukio tulikuwa naye kwenye ngoma usiku. Alikuwa
mchangamfu sana, aliifanya shughuli ipendeze.
“Ilipofika saa
nane usiku baadhi ya watu walianza kulala, sasa sijui yeye
ilikuwaje mpaka hali hiyo ikamfika maana hao watu walichomfanyia
wametuachia historia kubwa sana.
“Walimbaka wakaona haitoshi wakamwingiza chupa ya soda
sehemu ya siri ya mbele halafu wakamwingiza chupa ya bia
sehemu ya siri ya nyuma.
“Ili kuzidi
kutimiza unyama wao, waliondoka na kumwacha kama
alivyozaliwa, inauma sana halafu matukio ya hivyo yamekithiri
sana.”
Aliongeza: “Marehemu ametuachia jukumu la malezi kwa watoto
wake wawili, Sikudhani Juma (18) na Ally Juma (12).”
Naye mtoto mkubwa wa marehemu, Sikudhani akisimulia kifo cha
mama yake, alisema: “Nasikitika sikuweza kuuona mwili wa mama
hata pale watu walipojazana na kumshangaa.
“Hata polisi na mganga mkuu wa mkoa walipofika kumchomoa zile
chupa sikutaka kusogea kabisa, naamini Mungu atawaonesha jambo
hao watu hapahapa duniani.”
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Yurichi Mtei akizungumzia
ukatili huo alisema: “Taarifa za tukio hilo bado hazijafika kwangu
kutokana na majukumu mengine ya kikazi, isipokuwa nalifanyia kazi
kuhakikisha watuhumiwa wanakamatwa.”
Tukio hilo lilifunguliwa jalada kwenye Kituo cha Polisi Chalinze kwa
namba CH/RB/3767/2013 MAUAJI.
Mpaka kifo chake, mwanamke huyo alikuwa akiishi na mwanaume
mmoja (jina halikupatikana mara moja lakini si aliyezaa naye
watoto hao wawili). Alizikwa Jumapili iliyofuata, Chalinze.
Mungu ailaze pema peponi roho yake. Amina.

Share story hii kwa marafiki :

No comments:

Post a Comment

 
FOR WEB AND BLOG DESIGNERS : Call 0658184797
Copyright © 2011. AFRICA STEP - All Rights Reserved
Template Modify by Eddie Sucre
Proudly powered by Teknohama Tanzania