![Mwandamanaji mmoja akiwa ameinama karibu na nguruwe kwenye milango ya bunge tarehe 14 Mei wakati wa maandamano jijini Nairobi dhidi ya wabunge waliodai mishahara mikubwa. [Simon Maina/AFP]](http://sabahionline.com/shared/images/2013/05/14/kenya-pigs-mps-340_227.jpg)
![Waandamanaji wakiwa wamebeba mabango wakati wakiandamana kwenda bungeni huko Nairobi tarehe 14 Mei, 2013 wakipinga mpango wa wabunge wa kuongeza mishahara yao. [Tony Karumba/AFP]](http://sabahionline.com/shared/images/2013/05/17/kenya-protestors-salary-340_227.jpg)
"Hatutawaruhusu wabunge kujiongezea mishahara tukiwatazama tu," alipiga mayowe aliyepanga maandamano, Okiya Omtatah, kwa mujibu wa shirika la habari la AFP. "Ni waroho kama walivyo hawa nguruwe tuliowaleta hapa."
Polisi waliwakamata watu 10, wakatumia gesi ya machozi kuwatawanya waandamaji na kuwapiga wengine kwa magongo. Kisha walikimbia nyuma ya nguruwe hao waliotanda kwenye eneo lenye majani linalozunguka jengo la bunge.
Mnamo mwezi Machi, Kamisheni ya Mishahara na Ujira (SRC) ilikata mshahara wa wabunge isiyokatwa kodi kutoka shilingi 851,000 (dola 10,100) kwa mwezi hadi shilingi 535,000 (dola 6,400).


No comments:
Post a Comment