Habari Mpya :
Home » , » Mwanariadha wa Afrika kusini Oscar Pistorius amerejea tena mahakamani kuhojiwa zaidi na kujibu maswali ya mwendesha mashtaka mkuu Gerrie Nel katika kesi anayoshtumiwa kwa kumpiga risasi na kumuua mpenzi wake mwanamitindo Reeva Steenkamp nyumbani kwake mwezi februari tarehe 14 mwaka uliopita .

Mwanariadha wa Afrika kusini Oscar Pistorius amerejea tena mahakamani kuhojiwa zaidi na kujibu maswali ya mwendesha mashtaka mkuu Gerrie Nel katika kesi anayoshtumiwa kwa kumpiga risasi na kumuua mpenzi wake mwanamitindo Reeva Steenkamp nyumbani kwake mwezi februari tarehe 14 mwaka uliopita .

Imeandikwa na Shamsi Mohamed on Thursday, April 10, 2014 | 7:41 AM

Mwanariadha wa Afrika kusini Oscar Pistorius amerejea tena mahakamani kuhojiwa zaidi na kujibu maswali ya mwendesha mashtaka mkuu Gerrie Nel katika kesi anayoshtumiwa kwa kumpiga risasi na kumuua mpenzi wake mwanamitindo Reeva Steenkamp nyumbani kwake mwezi februari tarehe 14 mwaka uliopita .

Bwana Nel amekuwa akimwandama Pistorius , akisema hakuwa mkweli katika toba yake na alimfokea mpenzi wake Reeva Steenkamp mara kwa mara .
Siku ya kwanza ya maswali ya mahakama dhidi yake Nel alianza kwa kuonyesha picha za kutisha za kichwa kilichochuruzika damu cha Bi Steenkamp, baada ya kupigwa risasi na Pistorius.
Mwanariadha huyo anadai hakumuua makusudi bali alidhani ni mtu alievamia nyumba yake.
Ameiambia mahakama kuwa alimpenda sana mwanadada huyo Reeva .
Kiongozi wa mashataka amemsuta Pistorious akisema kuwa alikuwa ni mbinafsi sana kwa mpenzi wake na kuwa kile alichokijali sana ilikuwa ni sifa zake na hadhi yake katika jamii.
Pistorious alikanusha madai hayo akisema anajuta kwanini hakuwahi kumwambia Reeva kuwa anampenda kupitia ujumbe wa simu ya mkonon
 
Kiongozi wa Mashtaka Nel Gerrie 


Mwanariadha huyo alikuwa na wakati mgumu kuelezea mahakama kwanini Reeva alimlaumu kwa kumuonea katika moja ya ujumbe wa simu ya mkononi wa WhatsApp ambao alimwandikia Oscar''tangu turejee kutoka cape town
umekuwa ukinionea sana .''
Viongozi wa mashtaka wana imani kuwa alimuuwa kimakusudi ndani ya choo chake baada ya kuzozana.
Mwanariadha huyo mlemavu mwenye umri wa miaka 27, ambaye hana miguu yake yote mawili, huenda akahukumiwa jela maisha iwapo atapatikana na kosa la kuuwa.
Kinyume ya hali ilivyokuwa Siku ya Jumanne, alipolia kizimbani alipokuwa akielezea yaliyojiri nyumbani kwake kabla na baada ya mauwaji hayo,
leo alionekana mjasirii na mtulivu akimjibu Kiongozi wa mashataka ya umma bwana Nel.
Mamake Reeva bi June Steenkamp amesema kuwa japo aliombwa msamaha na Oscar moyo wake haukumsamehe kwani hadi hapo Oscar hakukiiri alimua bali alisisitiza kuwa anaomba msamaha kwa kusababisha kifo chake..

Pistorius akitoa ushahidi

Bi Steenkamp alishangaa iwapo Pistoriuos alikuwa anaigiza au la kwani amekuwa akilia na kutapika mahakamani .
Katika tukio lingine Oscar alikataa katakata kuwa alifyatua risasi katika mkahawa mmoja alipoulizwa na kiongozi wa Mashtaka bwana Nel.
Pistorious alisema kuwa hakujua bunduki hiyo ilikuwa na risasi.
Iwapo hatapatikana na hatia ya kukusudia kuua Reeva ,basi kulingana na sheria za Afrika Kusini, Pistorious huenda akashtakiwa kwa kosa la kuua bila ya kukusudia ambayo hukumu yake ni kati ya miaka 6- 15 jela.
Mbali na shtaka la mauaji, Pistorius anakabiliwa na shtaka la kufyatua bunduki hadharani na shtaka lingine la kumiliki risasi kinyume na sheria.

Bi Steenkamp mahakamani
Share story hii kwa marafiki :

No comments:

Post a Comment

 
FOR WEB AND BLOG DESIGNERS : Call 0658184797
Copyright © 2011. AFRICA STEP - All Rights Reserved
Template Modify by Eddie Sucre
Proudly powered by Teknohama Tanzania