Toka katika ofisi ya watetezi wa haki za binaadamu leo hii wametoa tamko lasmi kwamba Waziri mkuu bwana Mizengo Peter Pinda anatakiwa kubadilisha kauli aliyoitoa Alhamisi ya week mbili zilizopita bungeni Dodoma Kwamba'Kama mtu anakatazwa na hataki kusikia serikali imechoshwa na fujo polisi wapigeni wote watakao kiuka amri.Kauli hii aliitoa waziri mkuu bungeni Dodoma kufuatia fujo zilizotokea Arusha ambapo bomu lilipuliwa eneo mkutano wa Chama Cha chadema ulipokuwa ukifanyika na baadae fujo zilizoandamwa na Risasi na kipigo toka kwa askari dhidi ya wanachama wa Chadema na wafuasi wao ambapo baadhi ya viongozi wa chadema waliumizwa na baadhi ya wananchi kupoteza maisha.Wanaharakati na wasimamizi wa haki za binadamu kupitia Mtetezi wa haki za binadamu Prugensi Massawe ivyi leo wamemtaka Waziri mkuu kufuta kauli iyo aliyotoa na kusema kwamba Tanzania ni nchi inayoongozwa kwa sheria..
Home »
 » WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA ATAKIWA KUFUTA KAULI ALIYOITOA BUNGENI KUHUSU ASKALI KUWAPIGA RAIA WAFANYAO FUJO 
 

 
  

No comments:
Post a Comment