Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema kimemvua nyadhifa
zote Naibu Katibu mkuu wake Zitto Kabwe ambae ni mbunge wa
Kigoma Kaskazini.
Mwanasheria mkuu wa CHADEMA Tundu Lissu kwenye makao makuu
ya chama hicho, amesema Zitto na wenzake watatu wamebainika
kukihujumu chama kwa kuanzisha kitu kinaitwa Mkakati 2013
kinacholenga kukisambaratisha chama hicho ili kuwaondoa
madarakani Mwenyekiti na Katibu mkuu wake.
Nyadhifa alizovuliwa ni Unaibu katibu mkuu pamoja na Naibu
kiongozi wa upinzani bungeni ambapo yeye, Dr. Kitila Mkumbo na
Samson Mwigamba na mwingine mmoja Makao makuu wamepewa
siku kumi na nne wajieleze kimaandishi kabla ya kuchukuliwa hatua
zaidi za kinidhamu ikiwemo kuvuliwa Uanachama.
Home »
News
,
Politics
,
SIASA
» TUNDU LISSU ASEMA''ZITTO NA WENZAKE WATATU WAMEBAINIKA KUKIHUJUMU CHAMA


No comments:
Post a Comment