Kenya leo ikiwa ni tarehe 12 december imeadhimisha miaka 50 za uhuru tangu walipopata uhuru wao wabendera toka kwa mkolon wa kiingereza mnamo mwaka 1963 chini ya mwanaharakati wa uhuru na mkombozi wa Taifa ilo Mzee Jomo Kenyatta.Sherehe za uhuru zimeanza tangu usiku wa kuamkia Alhamis ambapo Bendera ya Taifa ilipandishwa katika viwanja vya Uhuru zoez ambalo lilishuhudiwa na rais Uhuru Kenyatta.Kwa upande wa wananchi wa kenya wengi wamesikika wakisema ni jambo la furaha kwao hasa wakikumbuka Historia ya Nchi yao chini ya mikono ya mkolon tangu mwaka 1875 kipindi ambacho kilikuwa cha ubaguzi,unyonyaji na mateso kwa wananchi kwa ujumla.Rais Uhuru kenyatta ambae kwa sasa anakabiliwa na mashtaka katika mahakama ya makosa ya kimataifa ya makosa ya jinai (ICC)amehutubia taifa leo kama alivyofanya baba yake Mzee Jomo kenyatta mwaka 1963 alipokuwa Rais wa kwanza kutawala Kenya na kuingoza jamuiya ya AFRICA MASHARIKI.
Baadae imeelezwa kwamba Bendera itapandishwa kilele cha mlima Kenya na wapanda milima kama ishara ya Uhuru katika Taia ilo.
 

 

No comments:
Post a Comment