Leo ikiwa ni Tarehe 14 december 2013 imewekwa katika historia ya dunia ikiwa ni Tarehe mwili wa Baba wa Taifa la Afrika ya kusini Mzee Nelson Mandela aliyefariki Tarehe 5 December 2013 kwa matatizo ya upumuaji katika mapafu ndo umepelekwa Rasmi kijijin kwake alipozaliwa na kukulia QUNU kwa ambapo anatalajiwa kuzikwa uko Kesho tarehe 15 december 2013 karibu na makaburi ya watoto wake watatu.
Hizi nishima za mwisho zilizotolewa na watu mbalimbali kabla ya mwili wa mandela kupelekwa Airport na viongozi wakuu ngazi ya Jeshi kuu na kupakizwa katika Dege la jeshi kuelekea Kijijin Qunu.
Ni baada ya safari wa muda mfupi hatimae mwili wa mandela umeweza kufika Qunu salama na kupokewa na Mamia ya wananchi waliojipanga barabaran kumpokea mwanaharakati uyo wa haki za binadamu aliyefungwa gerezan kwa kipindi cha miaka 27 na kisha kutoka na kuwa Rais wa kwanza mweusi Nchin Afrika ya kusini na mpingaji wa ubaguzi wa rangi.




No comments:
Post a Comment