Ijuma ya juzi ilikuwa ni siku ambayo (MFDI) au media for development international ilifungua sherehe za SwahiliWood kwa kuachia filamu mpya za kitanzania za kiswahili.Filamu tatu kati ya zile zilizoachiwa live
kwa rangi nzuri kabisa ni pamoja na SUNSHINE ambayo Star wake mkubwa ni msanii Ben Pol,zingine ni Mdundiko na NETWOK.Muungano huo wa Filamu za kiswahili wa SwahiliWood pia iyo siku uliweza kutamka rasmi juu ya hati miliki ya kazi za wasanii na kuwaomba wasanii wote Tanzania sio msanii wa BongoFlava na wale wa BONGOMOVIE kuungana na kuakikisha wasanii wa tanzania wanapata hatimiliki ya kazi zao.Kati ya wasanii wakongwe waliousindikiza usiku huo katika tasnia ya Filamu ni pamoja na Jb,Cheni,Shilole na Ray kigosi.


No comments:
Post a Comment