Taarifa zilizoelezwa katika kurasa mballimballi zinasema kwamba watoto watatu wamekutwa wamekufa uko
atamelang kaskazin magharibi.Polisi amesema maneno haya siku ya ijumaa kwamba babu wa kijana mmoja kati ya hao waliokutwa wamekufa aliikuta watoto hao wamekufa kkatiika friji siku ya ijumaa,Sergent Kealeboga Molale ameeleza kwamba watato hao wenye umri wa kati ya miaka mitatu na minne siku ya jumanne walikuwa wakicheza nje mwa nyumban kwao.Inaaminika kwamba watoto hao walijifungia katika Friji wakati wakicheza.Wazazi na ndugu na jamaa walijaribu kuwatafuta bila mafanikio na pia majirani walijulishwa na kusaidia kutafuta bila mafaniko pia lakin ilipofika siku ya ijumaa majira ya saa sita babu wa mmoja wa watoto alienda kufungua izo friji na kuwakuta watoto hao wamejifungia umo.
No comments:
Post a Comment