Hii ni promoshen inayochezeshwa na kampuni ya chapa ya Vodacom nchini Tanzania kwa upande wa huduma ya kutuma na kupokea pesa Iitwayo Mpesa.Promoshen hii iliyopewa jina la SHINDA MSHIKO KWA WAKALA imeanzishwa rasmi kwa ajili ya kuboresha huduma ya Mpesa kwa Vodacom kuwazawadia mawakala watano kila wiki katika kila jimbo baada ya droo ya kila wiki kuchezeshwa.Muwakilishi wa Jimbo la singida mjini,vijijin na wilaya zake Bw. Ayubu kalufya ameeleza kama ifuatavyo: Ni promotion ya mshiko kwa mawakala inarun kila wiki Mawakala watano wanapata kila mmoja laki moja kwenye kila territory so kwa singida ni tumepata mawakala kumi Na kila mmoja anapewa cheti.Pia kila territory anapatikana wakala bora ambaye anapata cheti cha uwakala bora japo hapati pesa yeye.Picha ni baadhi ya mawakala kati ya kumi walioshinda shilling 100,000 kila mmoja wakiwa wanakabidhiwa hundi zao na Bw.Ayubu kalufya akiwa na msaidizi wake wa jimbo la singida mjini upande wa M-pesa na na ukuaji wa biashara kwa ujumla Bw.Samson na wakala bora akiwa anakabidhiwa cheti chake cha uwakala bora.
No comments:
Post a Comment