Habari Mpya :
Home » » MAZIWA MATATU MKOAN MANYARA KUFUNGWA KUANZIA DECEMBER MPAKA JUNE 2014

MAZIWA MATATU MKOAN MANYARA KUFUNGWA KUANZIA DECEMBER MPAKA JUNE 2014

Imeandikwa na Shamsi Mohamed on Monday, November 25, 2013 | 10:00 AM

Uongozi wa mkoa wa manyara umetoa tangazo la kufungwa kwa maziwa matatu maarufu mkoan hapo kwa kipindi cha nusu mwaka kuanzia tarehe 1 December mpaka Tarehe 1 June mwaka mpya 2014.Kwa mujibu wa Mkuu wa mkoa wa Manyara Bw:Elaston Mbwilo amesema shughuli zote za uvuvi zinazoendelea katika maziwa taja hapa Ziwa Babati na ziwa Burunge yote ndani ya Wilaya ya Babati pamoja na ziwa Balangid ndani ya wilaya ya Hanang zitazuiwaa kwa kipindi cha nusu mwaka.Lengo la kufunga maziwa ayoo Mkuu wa mkoa amesema ni kutaka kurejesha hali ya mazingira katika usafi na kuyatunza pia kuacha samaki na viumbe wengine wa majini wapate kuzaliana kwa wingi na kuyaweka mazingira yanayozunguka maeneo ya maziwa katika hali nzuri ambapo kwa sasa yamealibiwa sana na shughuli za uvuvi.Mkuu uyo wa mkoa ameongezea kwamba maziwa hayo yanatoa samaki ambao wanauzwa Jamuhuri ya kidemocrasia ya Congo na utoa Ton 10,000 kwa mwaka mzima na kadirio la ton 1000 kwa kila mwezi ambapo samaki wengi uuzwa jijin arusha.

Share story hii kwa marafiki :

No comments:

Post a Comment

 
FOR WEB AND BLOG DESIGNERS : Call 0658184797
Copyright © 2011. AFRICA STEP - All Rights Reserved
Template Modify by Eddie Sucre
Proudly powered by Teknohama Tanzania