Leo majira ya Asubuhi katika Mlima wa saranda uliyopo nje kidogo ya wilaya ya Manyoni mkoani singida imetokea ajari baada ya Gari ndogo kuligonga trela la scania.Imeripotiwa kwamba gari ndogo iliyokuwa nyuma ya gari ilo kubwa imeshindwa kumiliki brake zake vizuri na kuligonga kwa nyuma trela ilo na kusababisha msongamano mkubwa uliosababisha foleni katika barabara iyo ya kutoka manyoni kuelekea Mkoan Dodoma.Taarifa zilizotufikia ni kwamba baada ya saa chache gari ilo dogo ambalo limearibika upande wake wa mbele liliweza kutolewa pemben na kuruhusu huduma za barabara iyo kuendelea.Hakuna aliyepoteza maisha wala majeruhi.


No comments:
Post a Comment