Habari Mpya :
Home » , , » BUSH NA CRINTON KUONGOZANA NA OBAMA KWENDA KATIKA MAZISHI YA MANDELA

BUSH NA CRINTON KUONGOZANA NA OBAMA KWENDA KATIKA MAZISHI YA MANDELA

Imeandikwa na Shamsi Mohamed on Sunday, December 8, 2013 | 6:52 AM

Toka ikulu ya Marekani imetangaza kwamba Rais Baraka Obama na mkewe first lady Michelle Obama watakwenda Nchini Afrika ya kusini kuudhulia mazishi ya Nelson Mandela,Rais mstaafu George W.Bush nae pia na mkewe Laura wametangaza kuongozana na Rais Obama kwenda katika mazishi ya Nguli uyo mtetezi wa haki za binadam aliywfariki tarehe 5 december baada ya kusumbuliwa na maradhi yaliohusisha matatizo ya upumuaji mzuri katika mapafu.

Kwa upande mwingine wa rais mstaafu Bill Crinton ambae wakati wa utawala wake hayati Nelson Mandela pia alikuwa madarakan pia ametangaza kuungana na rais Obama pamoja na mkewe Hillary Crinton kwenda afrika ya kusini kutoa heshima zao za mwisho kwa Kiongozi uyo aliyetumia muda mwingi wa maisha yake kupigania haki za binadam na kuondoa ubaguzi wa rangi uliokuwepo nchiniwake miaka ya Nyuma.Picha ya chini huu ndo uwanja ambao utatumika tarehe 10 december kwa ajili ya Dunia nzima kutoa heshima zao za mwisho(Memorial Service).

Share story hii kwa marafiki :

No comments:

Post a Comment

 
FOR WEB AND BLOG DESIGNERS : Call 0658184797
Copyright © 2011. AFRICA STEP - All Rights Reserved
Template Modify by Eddie Sucre
Proudly powered by Teknohama Tanzania