Habari Mpya :
Home » , , » MANDELA AAGWA NA MAELFU KATIKA(UNION BULDING)PRETORIA

MANDELA AAGWA NA MAELFU KATIKA(UNION BULDING)PRETORIA

Imeandikwa na Shamsi Mohamed on Thursday, December 12, 2013 | 4:21 AM

Mwili wa Mzee mandela jana ulitolewa rasmi Mochwali ya hospital ya kijeshi na kupelekwa moja kwa moja katika (UNION BULDING) katika mji mkuu pretoria afrika ya kusini.Rais jacob Zuma na familia ya Nelson Mandela wakiongozwa na Mke wa marehemu Mama Graca Michel walipata nafasi ya kwanza kuaga
mwili wa kiongozi uyo aliyefariki Alhamis ya wiki iliyopita kabla.Imerepotiwa kwamba mwili wa Mzee Mandela utatunzwa hapo kwa siku tatu kabla ya kwenda kuzikwa kijijin kwake Qunu.

PICHA:RAIS ZUMA NA GRACA MICHEL
Katika tukio ilo.la kihistoria baadhi ya viongozi waliopewa nafasi ya kuaga mwili huo wa shujaa na mtetezi wa haki za binadam ni pamoja na Rais wa jumuhuri ya muungano wa Tanzania Mh:Jakaya Mrisho kikwete na Rais wa Zimbabwe Robert mugabe na watu wengine maarufu dunian na baada ya wao lilifuata kundi la watu waliojipanga msururu kumuaga shujaa uyo.
PICHA:Rais Robert Mugabe na Mkewe
:Gari iliyobeba mwili wa Madiba
:Msafara ukisindikiza Mwili
:Mwili Uliingizwa(Union Bulding).
Imeripotiwa kwamba mahara hapa ndipo mzee mandela alipoapishwa mnamo mwaka 1994 alipokuwa Rais wa kwanza wa Taifa ilo la Afrika ya Kusini baada ya kutumikia kifungo cha miaka 25 gerezani chini ya utawala wa kikaburu.Mwili wa Mandela unatarajiwa kuzikwa kijijin kwao apo December 15.
R.I.P MANDELA
SOURCE:BONGO5.
Share story hii kwa marafiki :

No comments:

Post a Comment

 
FOR WEB AND BLOG DESIGNERS : Call 0658184797
Copyright © 2011. AFRICA STEP - All Rights Reserved
Template Modify by Eddie Sucre
Proudly powered by Teknohama Tanzania