Habari Mpya :
Home » » WALAJI WA NYAMA YA NGURUWE UENDA BAADAE WAKAPATA UGONJWA WA KIFAFA

WALAJI WA NYAMA YA NGURUWE UENDA BAADAE WAKAPATA UGONJWA WA KIFAFA

Imeandikwa na Shamsi Mohamed on Thursday, December 26, 2013 | 8:01 AM

Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) kimehadharisha walaji wa
nyama ya nguruwe nchini, kuwa wanakabiliwa na hatari ya kupata
kifafa.
Utafiti wa kisayansi uliofanywa na SUA, umebaini kuwa baadhi ya
nguruwe wana minyoo aina ya tegu ambao nyama yao ikiliwa bila
kuiva vizuri, mlaji atapata minyoo hiyo ambayo huingia kichwani na
kusababisha kifafa.
Akizungumza na mwandishi hivi karibuni, Mhadhiri na Mtafiti wa
Idara ya Sayansi ya Wanyama na Uzalishaji ya SUA, Profesa
Faustine Lekule, alisema sampuli za utafiti huo kutoka Mbeya,
zimebaini nguruwe wengi wakiwamo wanaosafirishwa katika miji
mikubwa wameathirika na minyoo hiyo.
Kwa mujibu wa Profesa Lekule, wataalamu wa SUA wanaosimamia
Mradi wa Utafiti wa Kuboresha Ufugaji wa nguruwe kwa mkoa wa
Mbeya ili kuinua pato la kaya, unaofadhiliwa na Shirika la Kimataifa
la Maendeleo la Denmark (DANIDA), walibaini hatari hiyo baada
ya kuchukua sampuli ya nyama ya nguruwe kwa ajili ya vipimo.
“Majibu ya sampuli ambazo wataalamu wamezichukua kutoka kwa
nguruwe wa wafugaji kwenye baadhi ya vijiji, wamebainika
kukumbwa na hatari hii.
“Lazima jitihada za makusudi zichukuliwe katika kutafuta ufumbuzi
wa pamoja wa tatizo hili kati ya watafiti na Serikali,” alisema
Profesa Lekule.
Alisema maambukizi ya tegu au minyoo ya nguruwe yanatokana na
tabia za baadhi ya wafugaji kutozingatia ufugaji bora kwa
kuwaacha kujitafutia chakula na maji mitaani na kula kinyesi cha
binadamu.
Kwa mujibu wa Profesa Lekule, baadhi ya wafugaji wamekuwa
wakijisaidia vichakani na kuwaacha nguruwe kutafuta malisho
katika vichaka na kula kinyesi chao, hali inayochangia ongezeko la
maambukizi ya minyoo ya tegu hao.
Baada ya kula kinyesi minyoo humwingia mwilini na kumdhoofisha
na baadaye binadamu anapokula nyama ambayo haijaiva vizuri,
minyoo hiyo humwingia na kusababisha kifafa baada ya kuingia
kichwani.
Alisema athari za kuenea kwa maambuziki hayo inaweza kutokea
katika miji mikubwa ikiwamo Dar es Salaam kwa kuwa nguruwe wa
Mbeya husafirishwa na kuuzwa maeneo hayo.
“Hatua hii inaweza kusababisha kusambaa kwa ugonjwa huu,
hivyo ushirikiano kati ya wafugaji, wafanyabiashara, Serikali na
wataalamu wa afya katika kufikia hatua ya kumaliza changamoto
hii unahitajika,” alibainisha Profesa Lekule.

Share story hii kwa marafiki :

No comments:

Post a Comment

 
FOR WEB AND BLOG DESIGNERS : Call 0658184797
Copyright © 2011. AFRICA STEP - All Rights Reserved
Template Modify by Eddie Sucre
Proudly powered by Teknohama Tanzania