Habari Mpya :
Home » , , » MAFIKIZOLO KUTENGENEZA VIDEO YA WIMBO WAO MPYA WENYE NENO LA KISWAHILI (NAKUPENDA)

MAFIKIZOLO KUTENGENEZA VIDEO YA WIMBO WAO MPYA WENYE NENO LA KISWAHILI (NAKUPENDA)

Imeandikwa na Shamsi Mohamed on Monday, April 7, 2014 | 5:48 AM














Kundi la muziki la Mafikizolo kutoka Afrika Kusini ambalo lipo nchini kwajili ya show moja itakayofanyika leo Mlimani City, lina mpango wa kufanya video ya wimbo wao mpya ‘Nakupenda’ hapa Tanzania kabla ya kuondoka.

“Tungependa kufanya video ya Nakupenda hapa Dar kwani jina la wimbo ni la kiswahili na itapendeza hivyo, bado hatujapata director wa kufanya video hii ila ndio mpango wetu”
Pia Mafikizolo wamesema wamefanya mabadiliko makubwa katika muziki wao ili kukidhi haja za bara zima la Afrika.

“mabadiliko ya muziki wetu yalifanyika ili kuteka soko la bara lote la Africa na zaidi ikiwezekana ndio maana Khona na Happiness zina miondoka tofauti”. Alisema Nhlanhla Nciza

Katika hatua nyingine Mafikizolo wamethibitisha kuwa wanampango wa kufanya kazi na msanii mkubwa kutoka Tanzania atakaye tajwa hivi karibuni na collabo hii ndio chanzo cha kuboresha mahusiano mazuri na wasanii wa Tanzania.
Share story hii kwa marafiki :

No comments:

Post a Comment

 
FOR WEB AND BLOG DESIGNERS : Call 0658184797
Copyright © 2011. AFRICA STEP - All Rights Reserved
Template Modify by Eddie Sucre
Proudly powered by Teknohama Tanzania