Habari Mpya :
Home » » MICHELLE OBAMA ASEMA ELIMU NDO MKOMBOZI WA MWANAMKE

MICHELLE OBAMA ASEMA ELIMU NDO MKOMBOZI WA MWANAMKE

Imeandikwa na Shamsi Mohamed on Sunday, July 7, 2013 | 5:39 AM

Katika ziara ya rais wa marekani afrika aliyongozana na familia yake kutembelea nchi tatu za afrika senegal,afrika ya kusin na kumalizia tanzania.Baada ya ziara iyo kumalizika api juzi yamefanyika mahohiano yaliyomuhusisha Michelle obama na mama Bush kuelezea hali halisi ya mwanamke wa afrika wake wa maraisi wa afrika na jinsi ya kumkomboa mtoto wa kike wa afrika.Michelle ameeleza kwamba jamii nyingi hasa jamii za kimarekani hazina muamko juu ya suala la elimu na kutoona thamani ya elimu.Amesema elimu ndo mkombozi wa maisha na kwamba elimu inatakiwa kutolewa sawa kwa jinsia zotee bila ubaguzi akitoa mfano wake yeye amesema"mimi nimezaliwa katika familia ya kawaida wazazi wangu hawakuwa matajiri lakin waliona umuhimu wa elimu wakanipeleka shule sawa na kaka zangu,akiongeza na kusema nisingekuwa first lady leo kama nisingesoma.Akuacha kumpongeza mama salma kikwete kwa juhudi zake za kuwaendeleza watoto wa kike na pia akawasihi wake wa maraisi wote kuwa mstari wa mbele kumuondoa adui ujinga katika familia zao hasa kwa mtoto wa kike..

Share story hii kwa marafiki :

No comments:

Post a Comment

 
FOR WEB AND BLOG DESIGNERS : Call 0658184797
Copyright © 2011. AFRICA STEP - All Rights Reserved
Template Modify by Eddie Sucre
Proudly powered by Teknohama Tanzania