Kampuni ya simu tanzania imeingia ubia na club yenye historia kubwa katika ulimwengu wa kambumbu dunian Manchester united katika kuendeleza vipaji na soka la vijana wa tanzania.Imeelezwa Airtel imeingia ubia huo wa kuileta club ya zaman ikiwa na wachezaji wa manchester wa zaman ambao wanatarajiwa kuingia Dar muda si mrefu.Afsa mahusiano wa club ya manchester Bw.Michael Higham amesema ni furaha kubwa kwake na club nzima kupata nafasi iyo kubwa na kuona ni kiasi gani wanakubalika na kusema kikosi cha wachezaji hao wakongwe wa Manchester watakuja tanzania kwa ajiri ya kufundisha na kukuza soka la tanzania.Japo hakuweza taja majina ya ni wachezaji gani wa zaman watakaokuja ila amesema wakiishaingia nchin kazi itakuwa moja tuu kutoa somo na hii itakuwa ni hatua kubwa kwa nchi ya tanzania alisema higham.Kwa upande wake Mkurugenzi mtendaji wa Airtel Bw.Sunil Colaso amesema ubia huo ni moja ya mafanikio ya soka la tanzania hasa kwa ngazi ya vijana.
No comments:
Post a Comment