Habari Mpya :
Home » , , » ZITUMIKE MALI ASILI ZA NCHI KUINUA MAISHA YA WATU WAKE ASEMA MKAPA,FESTUS NA OBASANJO

ZITUMIKE MALI ASILI ZA NCHI KUINUA MAISHA YA WATU WAKE ASEMA MKAPA,FESTUS NA OBASANJO

Imeandikwa na Shamsi Mohamed on Wednesday, November 20, 2013 | 3:25 PM

Serikali zimeshauriwa kutumia vyema mali asili zilizokatika nchi husika kuendeleza watu wake au kutoa fursa kwa wananchi kutumia mali asili zao kujiinua kimaisha na kukuza uchumi wa nchi husika.Wakizungumza juzi Dar es salaam viongozo teure wa mataifa matatu afrika rais mstaafu Benjamin Mkapa(Tanzania)Olesugen Obasanjo (Nigeria) na Dr Festus Magoe(Botswana) wamesema ni lazima wananchi wapewe kipaombele katika kuzitumia kwa ufasaha mali asili zao katika kukuza uchumi wao na wa taifa kwa ujumla.Mkutano ambao uliitishwa na kuwakutanisha watu mbalinbali mashuhuri akiwepo Mwenyekiti wa mashirika binafsi bwana Reginald Mengi ambae kwa upande wake alielekezea jicho lake kuwapa nafasi watanzania nafasi katika uchimbaji wa Oil na Gas,pia mkutano huo uliuzuriwa na ma chief mbalimbali wa serikali na sector binafsi,wawakilishi, mawaziri na pia Mkurugenzi mtendaji wa ITV/Radio one Joyce muhavile.Kwa upande wake obasanjo yeye alijaribu kutoa sababu zinasababisha umaskin kwamba ni Rushwa,hajira na migogoro ya Dini,pia amegusia kuhusu nchi yake kwa kusema kwamba Nigeria wameweka sheria inayompa kipaumbele mwananchi kuchimba oil na gas.

Share story hii kwa marafiki :

No comments:

Post a Comment

 
FOR WEB AND BLOG DESIGNERS : Call 0658184797
Copyright © 2011. AFRICA STEP - All Rights Reserved
Template Modify by Eddie Sucre
Proudly powered by Teknohama Tanzania