Mkurugenzi wa kampuni ya BenchMark Production Rita Paulsen au Madam Rita,amefunguka na kusema yeye ni miongoni mwa wanawake waliopata ujauzito wakiwa na umri mdogo lakini alikuwa jasiri kukabiliana na hali iyo mpaka akafanikiwa.Kupitia ukurasa wake wa facebook, Rita amewashauri wasichana wote wanaojikuta katika hali kama iyo kutokata tamaa kwa kuwa bado wanaweza kufanikiwa.
"Jambo msilolijua kuhusu mimi,nilipata ujauzito katika umri mdogo na kwa jamii yetu iliyotuzunguka ukizaa katika umri mdogo,watu huwa wanakunyanyapaa,hukuona hufai kuwa katika jamii na hata kukuhukumu.Kwa umri mdogo ule niliona kama hakuna maisha kwangu tena lakin sikukata tamaa na leo hii ujasiri wangu na kitu kinachonipa msukumo mpaka kufika hapa ndo icho kilichonikuta nikiwa na umri wangu mdogo.Kukata tamaa isiwe ndio chaguo lako la kwanza,"Aliandika Rita.


No comments:
Post a Comment