Wakatika wa tukio la kuupumzisha mwili wa aliyekuwa Rais wa kwanza mweusi na mkombozi wa Taifa la Afrika ya kusini zimeibuka shutuma kubwa toka kwa wananchi na wanakijiji cha Qunu baada ya kuzuiwa kuudhulia zoez zima la kumuaga na kumzika kiongozi wao uyo.Shutuma izo zimetokea baada ya serikali kutoa tamko kwamba Mandela ataagwa na watu walioalikwa tuu ili kuepusha msingamano na kudumisha aman katika zoe zima.Serikali apo hawali ilitoa tamko la kuwa na wagen 4000 tuu akiwemo Rais Jacob Zuma na Familia ya Mandela pamoja na marais waalikwa,marafiki wa familia ya Mandela na watu wengine na kusema wanakijiji na wananchi wengine hawatoruhusiwa kufika eneo husika la tukio la kumuaga na pia wakati wa kumzika bali watawekewa TV kubwa ili waweze kuona na kushiriki mazishi ya kiongozi wao.Kauli iyo imeleta tofauti na maana tofauti kwa baadh ya wanakijiji ambao wengi walisikika wakisema"Mandela ni mtu wetu na pia yeye akiwa hai hajawahi kubagua mtu iweje tukatazwe kumuaga na kumzika?"wananchi wengi hawajajitokeza kabisaa na wengine kujitokeza baada ya zoez la kuupeleka mwili wa MADIBA makaburin lilipoanza ndo wakasogea katika TV iyo na kuangalia kilichokuwa kinaendelea.Mbali na kuchukia kwa wanakijiji hao wameelezwa kwamba Mandela hakuwa kiongozi wao bali alikuwa kiongozi wa watu wote na sio rahisi kila mtu afike eneo la tukio lwa sababu ya usalama na mkusanyiko wa watu mashuhuri dunian.
Home »
Events
,
News
» WANANCHI WASEMA KUWEKEWA TV WAKATI WA MAZISHI YA MANDELA NI KITENDO CHA UBAGUZI
WANANCHI WASEMA KUWEKEWA TV WAKATI WA MAZISHI YA MANDELA NI KITENDO CHA UBAGUZI
Imeandikwa na Shamsi Mohamed on Sunday, December 15, 2013 | 6:38 AM
PICHA:Wananchi na wanakijiji wa QUNU ambao hawakuweza shuhudia tukio la mazishi ya mandela mojakwamoja wakifuatilia tukio ilo kupitia TV kubwa iliyowekwa mbali kidogo ya eneo mazishi yalipokuwa yakifanyika.


No comments:
Post a Comment