Msanii Naseeb Au Diamond platnum leo ametimiza ahadi yake aliyoitoa kwa watoto watakaoshinda katika shindano la kucheza Style yake mpya ya Ngololo baada ya kuwaandikisha watoto walioshinda na hapa Diamond ameandika ivyi katika mtandao wake wa ThisIsDiamond ***Napenda kumshukuru Mungu kwa kunipa fursa ya kuiona siku nyingine nikiwa na Afya njema kabisa,Mapema leo mchana,ilikuwa ni siku niliyopanga kutimiza ahadiyangu ya Kuwapeleka shule watoto walioshinda shindano la kucheza ngololo..na kwa vile nilitaka wapate elimu iliyo bora zaidi,nilikaa na management yangu..na kutafiti ni shule ipi itakayokidhi mahitaji ya watoto wale,shule yenye mazingira mazuri ya kusomea na yenye standard nzuri.sote tulikubaliana kuwapeleka shule ya EAST AFRICA INTERNATION SCHOOL,iliyopo Mikocheni.napenda kumshukuru mkuu wa shule hii,Bi Mercy Githirua kwa kutupokea vizuri mimi na watoto wale..lakini pia kuwashukuru wanafunzi wote kwa kutupokea vizuri**ayo ndo maneno ya diamond.
Home »
Events
,
Fashion
,
Music
,
News
» DIAMOND LEO AWAANDIKISHA SHULE WATOTO WALIOSHINDA KUCHEZA STYLE YA NGOLOLO
DIAMOND LEO AWAANDIKISHA SHULE WATOTO WALIOSHINDA KUCHEZA STYLE YA NGOLOLO
Imeandikwa na Shamsi Mohamed on Wednesday, January 22, 2014 | 11:52 AM
KATIKA PICHA:Msanii akisalimiana na walimu katika shulw ya East Africa International School.Akisalimiana na wanafunzi wa shule iyo.Picha nyingine ni mratibu shughuli nzima ya mshindi wa style ya Ngololo Simpo akiwa na washindi wawili ambao wanaenda kuandikishwa katika shule iyo kama ahadi ya Diamond.Washindi wakisoma sheria na kanuni za shule iyo na mwisho ni Shule yenyewe ya East Africa Internation School iliyopo Mikocheni jijin Dar es salaam.
Source:THISISDIAMOND


No comments:
Post a Comment