Habari Mpya :
Home » , , » DAVINA ASEMA NDOA IMEMFUNZA MAMBO MENGI!!

DAVINA ASEMA NDOA IMEMFUNZA MAMBO MENGI!!

Imeandikwa na Shamsi Mohamed on Wednesday, November 27, 2013 | 2:24 AM

                  Na Imelda Mtema
MSANII wa filamu za Kibongo, Halima Yahya ‘Davina’ amekiri kujifunza mambo mengi ya maisha baada ya kuingia kwenye ndoa.Akizungumza na mwandishi wetu, Davina alisema kwamba anaichukulia ndoa yake kama chuo cha mafunzo kwa jinsi alivyobadilika na kuwa tofauti na Davina aliyekuwa nje ya ndoa.“Nimekuwa tofauti kabisa na Davina wa kabla ya ndoa, sasa hivi kila kitu nakifanya kwa ustaarabu kwa kuwa najiona nimekuwa mwenye majukumu mengi,” alisema.Akifafanua zaidi, Davina alisema zamani alikuwa ni mtu wa kurandaranda hovyo tofauti kabisa na hivi sasa.“Zamani nilikuwa napenda safari zisizokuwa na faida tofauti na sasa hivi, kweli nimeamini ndoa ni chuo cha mafunzo,” alisema huku akiwaombea wasanii wenzake walio nje ya ndoa wafunge ndoa na kuwa na familia zao kwani watajifunza mengi.

Share story hii kwa marafiki :

No comments:

Post a Comment

 
FOR WEB AND BLOG DESIGNERS : Call 0658184797
Copyright © 2011. AFRICA STEP - All Rights Reserved
Template Modify by Eddie Sucre
Proudly powered by Teknohama Tanzania